TAWA YAWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI MBELE YA WAZIRI KIJAJI

TAWA YAWASILISHA TAARIFA YA UTENDAJI MBELE YA WAZIRI KIJAJI

Na Beatus Maganja, Dodoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imewasilisha taarifa ya utendaji wake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika kikaokazi kilichofanyika Oktoba 8, 2026bjijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Wizara kuelekea vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii vinavyotarajiwa kuanza Oktoba 13, 2026.

Kikaokazi hicho kimezikutanisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kupitia taarifa za utendaji wa mwaka wa fedha 2025/26 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/27 huku Waziri Kijaji akipitia maudhui yanayotarajiwa kuwasilishwa mbele ya Kamati hiyo.

Katika uwasilishaji huo, TAWA imeeleza utekelezaji wa majukumu yake ya usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori nchini, ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kufanikisha malengo ya Wizara katika sekta ya maliasili na utalii.

Maandalizi hayo yanalenga kuhakikisha taarifa zitakazowasilishwa mbele ya Kamati ya Bunge zimeandaliwa kwa usahihi na kuzingatia maeneo muhimu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi husika sambamba na kuimarisha uratibu wa shughuli za Wizara.