TAWA Kanda ya Kati yaendelea kuimarisha huduma za kijamii kupitia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kupitia Pori la Akiba Muhesi ilikabidhi mifuko 71 ya saruji kwa Shule ya Msingi Mitundu B kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa majengo mawili ya madarasa yanayoendelea kujengwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, iliyofanyika Mei 22, 2026, Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mitundu, Bi. Utukufu L. Gwimile, aliishukuru TAWA Kanda ya Kati kupitia Pori la Akiba Muhesi kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayozunguka maeneo ya uhifadhi, hatua inayochochea na kuimarisha ujirani mwema kati ya jamii na taasisi hiyo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Uhifadhi wa Pori la Akiba Muhesi alisisitiza umuhimu wa jamii kuendelea kushirikiana TAWA katika juhudi za uhifadhi wa maliasili, akieleza kuwa ushirikiano huo una mchango mkubwa katika kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii na hivyo kusaidia kuboresha huduma mbalimbali za kijamii.






