KAMPUNI YA ADAM CLEMENTS SAFARIS LTD  NA MAKAME  WMA ZAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SERENGETI AWARDS

KAMPUNI YA ADAM CLEMENTS SAFARIS LTD  NA MAKAME WMA ZAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA SERENGETI AWARDS

Na. Joyce Ndunguru, Arusha.

Kampuni ya uwindaji ya Adam  Clement  Safaris Ltd  imeibuka kidedea katika kategori  ya kampuni bora za Uwindaji  (Best Hunting Operator Company) katika Usiku Wa Tuzo Za  “The Serengeti Awards” Zilizofanyika tarehe 31 Januari, 2026 katika Ukumbi wa Mount Meru Hotel- Arusha. 

Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA, Mlage Yussuf Kabange. 

Dhima kuu ya tuzo hiyo ni  kutambua mchango wa Kampuni ya Adam Clements Safari katika sekta ya Utalii wa uwindaji ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii na taifa kwa ujumla.

Kadhalika, Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Makame ( Makame WMA) imeibuka mshindi katika kategori “Best  Wildlife Management Area award” 

Makame WMA imeibuka kidedea katika tuzo hizo ambapo imekuwa mstari wa mbele katika kuendeleza Uhifadhi na utalii nchini Tanzania. Jumuiya ya Hifadhi ya Makame imekuwa na mchango katika kuhakikisha kuwa jamii zinapata manufaa ya moja kwa moja kutoka kwa rasilimali zao, na kusaidia katika kuboresha hali zao za kiuchumi na maendeleo ya jamii. 

Aidha, Makame WMA imekuwa inasaidia kulinda korido za wanyamapori, kupunguza shughuli haramu, na kudumisha bayoanuwai inayozunguka hifadhi hiyo.