CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA WATEMBELEA MAKUYUNI WILDLIFE PARK

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA WATEMBELEA MAKUYUNI WILDLIFE PARK

Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) leo April 30, 2024 wametembelea Makuyuni Wildlife Park iliyopo wilaya ya Monduli katika mkoa wa Arusha kwa lengo la  kujifunza Uhifadhi wa wanyamapori na kujionea shughuli za Utalii.

Ziara hii ya mafunzo imefanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa  "Tuhifadhi Maliasili" unaoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET)  kwa ufadhili wa shirika la misaada la Marekani (USAID).

Mojawapo ya malengo ya Mradi huu ni kuokoa shoroba za wanyamapori zilizoathirika na uvamizi wa binadamu. Na Makuyuni ikiwa ni sehemu ya ushoroba wa Ziwa Manyara/Tarangire ilikuwa ni sehemu sahihi kupatembelea.

Waandishi  hao wapatao Saba (7) wakitokea vyombo vya habari vya Clouds Tv na Redio,  magazeti ya Nipashe, Zanzibar Leo,  Daily news na The guardian, walifurahia madhari nzuri ya Makuyuni Wildlife Park na kujionea wanyamapori kama vile Twiga, pundamilia, pofu, Nyati, Ngiri, Swala, Tembo, Greater Kudu. Pamoja na ndege kama vile kanga, tumbusi, njiwa n.k. Na wameahidi kurudi tena na kuwa mabalozi wazuri wa Makuyuni Wildlife Park katika vyombo vya habari wanapotokea.