TAWA YAPOKEA MELI ZA KIMATAIFA ZA WATALII KATIKA HIFADHI YA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA

TAWA YAPOKEA MELI ZA KIMATAIFA ZA WATALII KATIKA HIFADHI YA KILWA KISIWANI NA SONGO MNARA

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepokea meli mbili za Kimataifa kutoka nchi ya Australia na Ufaransa zilizotia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia ya Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara kwa lengo la kufanya utalii wa malikale na fukwe. 

Meli ya kwanza iitwayo Coral Geographer kutoka nchini Australia  ilibeba watalii 120 na meli ya pili iitwayo Le Jacques - Cartier Ponant  kutoka nchini Ufaransa ilibeba watalii 125.  

Mapokezi ya meli hizi za watalii yameratibiwa na Kampuni kubwa duniani ya Abercrombie and Kent kwa kushirikiana na TAWA.