TAWA YAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA

TAWA YAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA)  leo tarehe 10 Septemba, 2022 imekutana na kufanya kikao kazi na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika Pori la Akiba Pande lililopo jijini Dar es Salaam. Lengo la kikao kazi hiki ni kuendelea kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na vyombo vya habari kwa kuzingatia  umuhimu na nafasi ya vyombo vya habari katika kuendeleza uhifadhi wa rasilimali ya wanyamapori na shughuli za utalii nchini.