TAARIFA KWA UMMA
KUWASILISHA MAOMBI YA LESENI YA BIASHARA YA NYARA (TROPHY DEALER’S LICENCE – TDL) KWA MWAKA 2022
Wizara ya Maliasili na Utalii inawajulisha wananchi wenye nia ya kufanya Biashara ya Nyara kuwasilisha maombi yao kwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA). Fomu za Maombi ya Leseni zinapatikana katika Ofisi za Wanyamapori za Wilaya. Fomu hizo pia zinapatikana kwenye ofisi za TAWA Makao Makuu Morogoro (Jengo la TAFORI), Ofisi za Utalii na Huduma za Biashara, Dar es Salaam (Gorofa ya 4, Jengo la Mpingo) na ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori - Arusha zilizopo karibu na ofisi za jeshi la Zimamoto.
Fomu za maombi zinatakiwa kujazwa kwa usahihi, kuwasilishwa na kupitishwa na Maafisa Wanyamapori wa Wilaya. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Novemba, 2021.