Skip to main content

KUWASILISHA MAOMBI YA LESENI YA BIASHARA YA NYARA (TROPHY DEALER’S LICENCE – TDL) KWA MWAKA 2020

Wizara ya Maliasili na Utalii inawajulisha wananchi wanaotaka kufanya Biashara ya Nyara kuwasilisha maombi yao kwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania. Mwombaji atatakiwa  kujaza Fomu za Maombi ya Leseni zinazopatikana na kupitishwa na Maafisa Wanyamapori wa Wilaya husika. Fomu hizo pia zinapatikana kwenye ofisi za TAWA Makao Makuu Morogoro (Jengo la TAFORI), Ofisi za Utalii na Huduma za Biashara, Dar es Salaam (Gorofa ya 4, Jengo la Mpingo) na ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori -  Arusha zilizopo karibu na ofisi za jeshi la zima moto.

 

Fomu za mwombaji zinatakiwa kujazwa na kuwasilishwa kwa Maafisa Wanyamapori wa Wilaya ndani ya siku 45 tangu tarehe ya tangazo hili.

 

Hakuna Leseni za Daraja lolote kwa mwaka 2020 zitakazotolewa kwa madhumuni ya Ukamataji kwa ajili ya usafirishaji wa Wanyamapori hai nje ya nchi.

 

Maombi ya Leseni kwa Mwaka 2020 ni kwa Madaraja yafuatayo:-

 

Daraja

 Maelezo

1

Biashara ya meno ya kiboko au ngiri mazima au kipande ambayo hayajatengenezwa.

2

Biashara ya ngozi za wanyamapori isipokuwa ngozi za pimbi na mbega

3

Biashara ya ngozi za pimbi

4

Biashara ya meno ya kiboko na ngiri ambayo yamenakishiwa

5

Biashara ya kukata na kutengeneza ngozi za chui, simba, mondo au ngozi nyingine za wanyamapori jamii ya paka

6

Biashara ya kukata na kutengeneza ngozi za wanyamapori isipokuwa pimbi na mbega pamoja na kutengeneza vitu kutokana na nyara hizo

7

Biashara za nyara zilizotengenezwa

8

Biashara ya kuhifadhi nyara mbalimbali ili zisiharibike mapema

10

Biashara ya mikia ya wanyamapori isipokuwa ya tembo, faru, na mbega na vitu vinavyotokana na nyara hizo.

11

Wakala wa kusafirisha nyara kwa ujumla isipokuwa wanyamapori hai

12

Biashara ya ndege waliokaushwa na kutengenezwa

15

Biashara ya reptilia waliokaushwa na kutengenezwa

17

Bustani ya Wanyamapori

18

Mashamba ya kufuga wanyamapori (isipokuwa kwa nia ya kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi).

19

Vituo vya karantini (isipokuwa kwa nia ya kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi).

20

Ranchi za wanyamapori (isipokuwa kwa nia ya kusafirisha wanyamapori hai nje ya nchi)

21

Aina yoyote ya biashara ya Nyara ambayo haikutajwa kwenye daraja la 1-20 isipokuwa kwa nia ya kusafirisha viumbe hai nje ya nchi.

 

Mwombaji anatakiwa kuwasilisha fomu ya maombi ya leseni pamoja na uthibisho wa yafuatayo:-

1.     Endapo mwombaji ni mtu binafsi anatakiwa awasilishe hati ya usajili wa jina la biashara (Certificate of Registration of Business name) au iwapo mwombaji ni Kampuni awasilishe hati ya Kampuni (Memorandum and Articles of Association) na Hati ya utambulisho wa mlipakodi (Taxpayer Identification Number).

2.     Uthibitisho wa kuwa na wakamataji wenye elimu ya uhifadhi wa wanyamapori kutoka kwenye Chuo kinachotambulika na Serikali.

3.     Uthibitisho kwamba biashara ina Leseni kutoka kwenye Mamlaka husika.

4.     Mpango wa biashara [Business plan] unaohusu biashara inayotarajiwa kufanywa na uthibitisho wa kuwa na mtaji wa kufanya biashara hiyo.

5.     Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi ya leseni ya (TZS 5,000) ambayo haitarudishwa [Non- Refundable]. Fedha hizo zilipwe kupitia Akaunti ya TAWA CRDB  015031956610 kwa malipo ya fedha za Kitanzania na 0250319566100 kwa malipo ya Dola za Kimarekani (USD). NBC akaunti Na. 012103011903 kwa malipo ya fedha za Kitanzania (TZS) na Akaunti Na. 012105021353 kwa malipo ya Dola za Kimarekani (USD)

6.     Mwombaji asiwe na rekodi ya kupatikana na hatia ya kuvunja Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009.

7.     Kwa waombaji wa shughuli za ufugaji wa wanyamapori, ada ya maombi ya Leseni ya ufugaji itategemea aina ya mradi wa ufugaji  kama ifuatavyo:-

                                        i.          Bustani ya wanyamapori; ada ni Dola za Kimarekani 150 kwa mzawa, mzawa pamoja na Mgeni Dola za Kimarekani 250

                                      ii.          Mashamba ya ufugaji wanyamapori; ada ni Dola za Kimarekani 200 kwa mzawa na kwa mzawa na mgeni ni Dola za Kimarekani 500

                                     iii.          Ranchi ya wanyamapori ni Dola za Kimarekani 500 kwa mzawa na kwa mzawa na mgeni ni Dola za Kimarekani 1000

 

Imetolewa na.

KAMISHNA WA UHIFADHI

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA,

Barabara ya Dar es Salaam,

Eneo la Kingolwira, Jengo la TAFORI,

S.L.P 2658,

MOROGORO

Simu: 023-2934204

Barua pepe: cc@tawa.go.tz