Kanuni za Biashara ya Nyara za mwaka 2010, na Kanuni ya Usimamizi wa Maeneo ya Ufugaji Wanyamapori za mwaka 2020, zinatoa fursa kwa Watanzania kuwasilisha maombi ya Leseni za Biashara ya Nyara pamoja na usajili wa maeneo ya ufugaji wa wanyamapori. Hivyo katika kipindi cha Octoba- Disemba 2020, Mamlaka ilipokea maombi 103 ya leseni za biashara ya nyara ambapo maombi 98 kati ya hayo ndiyo yaliyokidhi vigezo vya kupata leseni kama ifuatavyo;