Wizara ya Maliasili na Utalii inawajulisha wananchi wanaotaka kuanzisha miradi ya ufugaji wanyamapori katika Bustani (Zoo/Sanctuary), Mashamba (Farms/Breeding Sites) na Ranchi (Ranch) au kuanzisha Eneo la Wanyamapori Yatima (Wildlife Orphanage facility) kuwasilisha maombi yao kwa Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania. Mwombaji atatakiwa kujaza Fomu za Maombi ya Usajili na Leseni zinazopatikana kwenye ofisi za TAWA Makao Makuu Morogoro (Jengo la TAFORI), ofisi za Utalii na Huduma za Biashara, Dar es Salaam (Gorofa ya 4, Jengo la Mpingo) na ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori - Arusha zilizopo karibu na ofisi za jeshi la zima moto.